Afrika: Fanya Upatikanaji wa Elimu wa Wasichana kuwa Kweli

Mamilioni ya wasichana wajawazito na walioolewa katika nchi nyingi za Afrika wananyimwa elimu kwa sababu ya sera na mienendo ya kibaguzi, Human Rights Watch wamesema leo katika siku ya Mtoto wa Afrika. Zaidi ya wasichana milioni 49 wameacha shule za msingi na sekondari Kusini mwa Jangwa la Sahara, ambapo milioni 31 kati yao wako nje ya elimu ya sekondari jambo ambalo linadhoofisha haki zao na kukwamisha fursa zao.

News