• Africa
    Mamlaka nchini Kenya imetekeleza unyanyasaji unaofanyiwa waandishi wa habari wanaoripoti maswala tata, hatua inayotishia uhuru wa kujieleza wakati ambapo taifa hilo linakaribia uchaguzi mkuu mnamo mwezi Agosti 8 2017 kulingana na ripoti iliotolewa na shirika la haki za kibinaadamu la Human Rights Watch na ofisi ya Shirika la ARTICLE 19 ya Afrika Mashariki. Waandishi wa habari pamoja na wanablogu wanaoripoti kuhusu maswala ya ufisadi, unyakuzi wa ardhi, operesheni za kukabiliana na ugaidi pamoja na ghasia za baada ya uchaguzi wa mwaka 2007-2008 pamoja na maswala mengineyo wamekabiliwa na vitisho, kupigwa pamoja na kupoteza kazi.