Skip to main content

Afrika Mashariki: Uhuru wa Kiraia Unapungua

Viongozi wa Kanda Wanapaswa Kuacha Ukandamizaji, Watoe Haki

(Nairobi)– Mlolongo wa ukandamizaji wa wazi wa serikali dhidi ya waandamanaji wa amani, wanaharakati, na waandishi wa habari uliibuka katika ukanda wote wa Afrika Mashariki na Pembe ya Afrika mnamo mwaka 2018, shirika la kutetea haki za binadamu Human Rights Watch limesema leo katika ripoti yake Ripoti ya Ulimwengu ya 2019. Serikali katika kanda hizi wanapaswa kuongeza juhudi katika kulinda uhuru wa kujieleza na kukusanyika, na kutoa haki kwa uhalifu unaofanywa na vyombo vya ulinzi vya serikali

Katika migogoro inayoendelea nchini Sudan, Sudan Kusini, na Somalia, majeshi ya kitaifa na makundi mengine yenye silaha yaliwalenga raia. Mapigano yamewaondoa mamilioni ya watu katika makazi yao wanayoishi katikati na mipakani mwa nchi zao. Ethiopia iliibuka kinara mwaka huo kama mfano wa mabadiliko chanya, yakiongozwa na Abiy Ahmed, ambaye aliteuliwa kuwa Waziri Mkuu mnamo mwezi Aprili, na kutekeleza mabadiliko mengi muhimu.


“Tunashuhudia uporomokaji wa kutisha kwenye haki za binadamu Afrika Mashariki na Pembe ya Afrika ambapo serikali zikitumia nguvu na ukandamizaji kuwanyamazisha wakosoaji wa amani na kushindwa kutekeleza uwajibishaji kwa uhalifu unaofanywa na vyombo vyake vya usalama,” amesema Mausi Segun, Mkurugenzi wa Afrika, Human Rights Watch. “Ethiopia imeonekana kuwa mfano wa kuigwa kwa kuwa tofauti na ukandamizaji huu.”

Katika Ripoti ya Ulimwengu yenye kurasa 674, ambayo ni ripoti ya 29, Human Rights Watch utekelezwaji wa haki za binadamu katika nchi zaidi ya 100. Katika ujumbe wa utangulizi, Mkurugenzi Mtendaji Kenneth Roth anasema kwamba viongozi wanaosambaza chuki na tabia ya kutokuvumiliana wanahamasisha upingwaji. Muungano mpya wa serikali zinazoheshimu haki za binaadamu, mara nyingi zikitiwa moyo na kuungwa mkono na makundi ya kiraia na umma kwa ujumla, wanafanya uongozi wa kiimla kuwa mgumu zaidi. Kufanikiwa kwa muungano huu kunaonesha uwezekano kwa kulinda haki za binaadamu – naam, wajibu wa kufanya hivyo – hata katika nyakati zisizo na nuru.

Nchini Ethiopia, Waziri Mkuu Abiy alitangaza azma yake ya kuondoa sheria kandamizi, kuondoa hali ya hatari, kuwaachia huru makumi ya maelfu ya wafungwa wa kisiasa, kubatilisha makatazo yaliyolenga vyama vya siasa vya upinzani na kuwafuta kazi viongozi kandamizi. Baadhi ya magereza ambazo kwa muda mrefu zilikuwa zimegubikwa na ukandamizaji, ikiwa ni pamoja na gereza la Ogden, yalifungwa, na hatua zikachukuliwa kuongeza uhuru wa taasisi muhimu, ikiwa ni hatua muhimu kuelekea uchaguzi wa kitaifa wa mwaka 2020.

Nchini Kenya, vyombo vya usalama vilitumia nguvu kuwasambaza waandamanaji wakati wa uchaguzi wa mwishoni mwa 2017 na mwanzoni mwa 2018. Usambazaji huo, ambao ulifanywa zaidi katika ngome za upinzani, uliua zaidi ya watu 100, na wanawake na wasichana kadhaa waliripoti kufanyiwa vitendo vya unyanyasaji wa kingono. Mamlaka za Kenya pia ziliwalenga waandishi wa habari wakati wa uchaguzi kwa kuripoti mada nyeti kama vile rushwa na usalama na kuwanyamazisha maofisa wa haki za binadamu waishio Nairobi na Kenya Magharibi kwa vitendo vya ukamatwaji wa ghafla, vitisho na kuvamiwa katika nyumba na ofisi zao.

Japo mamlaka inayosimamia utendaji kazi wa polisi (Independent Policing Oversight Authority (IPOA)), ilisema imeanza uchunguzi dhidi ya mauaji yanayodaiwa kutekelezwa na polisi, Human Rights Watch ilibaini kwamba hakuna afisa yeyote wa polisi aliyechukuliwa hatua kwa vitendo vya kihalifu vilivyofanywa na vyombo vya usalama.

Vyombo vya usalama vya Uganda pia viliwasambaza waandamanaji kwa kutumia nguvu; vikiwapiga, kuwaweka ndani visivyo halali, na nyakati zingine kuwatesa waandamanaji, waandishi wa habari na wanasiasa wa vyama vya upinzani. Watu thelathini na nne, ikiwa ni pamoja na wabunge, walikamatwa katika kampeni za uchaguzi mdogo Arua, magharibi-kaskazini mwa Uganda na kushtakiwa kwa uhaini, inadaiwa pia kuwa waliteswa na vyombo vya usalama. Pamoja na ahadi ya serikali kuvichukulia hatua vyombo vya usalama, Human Rights Watch iligundua kwamba chunguzi nyingi zilizogusa unyanyasaji uliofanywa na jeshi au polisi zilishindwa kuendelea, ikiwa ni pamoja na mashtaka ya mauaji ya Novemba 2016  ambapo zaidi ya raia 100 waliuwawa.

Tanzania imeonesha kuporomoka katika uzingatiaji wa uhuru wa kujieleza, kujumuika na kukusanyika tangu uchaguzi wa Rais John Magufuli mwaka 2015, pamoja na ukiukwaji wa haki zingine za binadamu. Mamlaka zimewafanyia unyanyasaji na kuwakamata waandishi wa habari, wanachama wa vyama vya upinzani na wanaharakati; na kutumia kauli za kikatili dhidi ya makundi madogo ya kijinsia, wakitishia kuwakamata watuhumiwa wote wa mapenzi ya jinsia moja na kuwafanyia uchunguzi wa njia ya haja kubwa wa lazima na kuwapatia ushauri nasaha wa kuwabadilisha maumbile yao. Wasichana wanakumbana na ubaguzi shuleni kufuatia katazo la mwaka 2017 kwa wasichana wote waliopata ujauzito na wale ambao wamejifungua kurudi shuleni.

Nchini Sudan, vyombo vya usalama vya serikali vilishambulia na kuharibu vijiji kadhaa eneo la Jebel Mara, katikati ya Darfur, na kuwalazimisha maelfu ya watu kukimbia eneo hilo. Khartoum na maeneo mengine, vyombo vya ulinzi vilitumia nguvu kuwatawanya waandamanaji na kuwakamata wanaharakati, waandishi wa habari, bloga na wanasiasa wa upinzani, huku wakitengenezea mashataka yenye adhabu za vifo kwa wanaharakati. Rais Omar al-Bashir amekwepa haki dhidi ya uovu alioufanya Darfur, na Sudan imepiga aidha hatua ndogo sana au kutokupiga hatua yoyote ile juu ya kuhusiana na uwajibikaji.

Sudan ya Kusini, mapigano dhidi ya serikali na waasi yanaendelea hata baada ya juhudi za makubaliano ya amani yaliyotiwa sahihi mwezi Septemba. Majeshi ya serikali yalitekeleza mashambulizi ya kikatili dhidi ya waasi katika maeneo ya magharibi ya Wau; wakiua, kupora, na kuharibu vijiji, huku vitendo vya unyanyasaji wa kingono vikishamiri katika jimbo la Unity. Viongozi wa serikali hawajapiga hatua yoyote ile baada ya makubaliano ya kutengeneza mahakama ya ushirika wa Umoja wa Afrika na Sudani ya Kusini ambayo ingeshughulikia kesi za ukatili wa hali ya juu kufanyika tangu kuanza kwa vita miaka mitano iliyopita.

Nchini Somalia, mapigano, ukosefu wa usalama, ukosefu wa ulinzi wa serikali, na kuzorota kwa misaada ya kibinadamu vimekuwa na madhara makubwa kwa raia mnamo mwaka 2018. Vyombo vya usalama viliua raia kinyume na sheria na kujeruhi raia wakati wa mapigano ya kugombania ardhi na vituo vya barabarani, na unyang’anyi wa silaha kwa waasi, hasa katika maeneo ya Mogadishu na Shabelle ya Chini. Kulikuwa na mashambulio yaliyolenga vyombo vya habari, ikiwa ni pamoja na unyanyasaji, na ukamatwaji wa kinyume na sheria, huku mamlaka zikifumbia macho uchunguzi wa mauwaji au mashambulizi dhidi ya waandishi wa habari. Serikali haijapiga hatua yoyote ile katika kushughulikia vyombo vya usalama vinavyofanya uhalifu, kama vile taasisi ya usalama wa taifa fighting, au kuachana na kuwaondoa watu ambao wamekimbia makazi yao.

Eritrea makubaliano ya amani ya Julai pamoja na Ethiopia na kuondolewa kwa vikwazo vya Umoja wa Mataifa mwezi Oktoba vilipelekea matumaini kwamba utawala kandamizi juu ya haki za msingi za binadamu ungeondolewa, lakini palikuwa na mabadiliko madogo sana mwaka 2018. Nchi haina vyombo vya habari huru, asasi za kiraia zilizo rasmi, vyama vya siasa au mahakama, na ukamatwaji kinyume cha sheria bado unaendelea kufanyika kama kawaida. Wananchi wanalazimishwa kujiunga na jeshi la kujenga taifa kwa kipindi kisichojulikana, mara nyingi katika jeshi la wananchi, na maelfu wanakimbia Eritrea kila mwezi.

Your tax deductible gift can help stop human rights violations and save lives around the world.