Skip to main content

Afrika: Wasichana Wajawazito, Kina Mama Vijana Wazuiwa Shule

Serikali za Afrika Zinapaswa Kuhakikisha Haki ya Kupata Elimu

“Evelina,” 17, na mtoto wake wa miaka 3 “Hope,” katika kaunti ya Migori, magharibi mwa Kenya. Evelina yuko kidato cha 2, mwaka wa pili wa shule ya sekondari ngazi ya chini. Baada ya mtoto wake kuzaliwa, rafiki yake alimhamasisha kurudi shule. Ijapokuwa Evelina hawezi kumudu kulipa ada, mwalimu mkuu wa shule amemkubalia kuendelea na shule. © 2018 Smita Sharma kwa ajili ya Human Rights Watch

(Nairobi) –  Maelfu ya wasichana wajawazito na kina mama vijana wanazuiwa au kukatishwa tamaa kuhudhuria shule barani Afrika, shirika la Human Rights Watch limesema katika ripoti iliyotolewa leo, kuelekea Siku ya Mtoto wa Afrika (Day of the African Child) Juni 16, 2018.



Ripoti ya kurasa 40, “Hakuna Kumuacha Nyuma Msichana Afrika: Ubaguzi katika Elimu dhidi ya Wasichana Wajawazito na kina Mama Vijana,” inatokana na utafiti wa kina wa shirika la Human Rights Watch juu ya haki za wasichana Afrika. Human Rights Watch waliangazia sheria za kitaifa, sera na taratibu ambazo zinaweka vikwazo au kuunga mkono haki za wasichana wajawazito na kina mama vijana kupata elimu ya msingi na sekondari katika nchi zote wanachama wa Umoja wa Afrika (AU). Afrika ina kiwango kikubwa cha mimba za ujanani duniani. Serikali za Afrika hazina budi kuharakisha sheria na sera kuhakikisha shule zinaruhusu na kusaidia wasichana wajawazito kuendelea na shule na kurudi shule baada ya kujifungua.

“Katika nchi nyingi za Afrika, wasichana wajawazito na kina mama vijana hufukuzwa shule na kunyimwa haki zao za kupata elimu,” anasema Elin Martínez, mtafiti wa haki za watoto na Shirika la Human Rights Watch. “Wakati kuna maendeleo kiasi fulani, umoja wa Afrika unahitaji kufanya kazi kwa karibu na nchi wanachama kuhakikisha kwamba hakuna msichana anaenyimwa haki ya kupata elimu kwa sababu ya kupata ujauzito.”



Katika miaka ya karibuni, serikali nyingi za Afrika zimeweka nia ya dhati kuhakikisha kwamba msichana mjamzito na mama wanaweza kuhudhuria shule. Hata hivyo, Guinea ya Equatoria, Sierra Leone na Tanzania bado zimepiga marufuku wasichana wajawazito au kina mama vijana kuhudhuria shule za umma.
“Evelina,” 17, na mtoto wake wa miaka 3 “Hope,” katika kaunti ya Migori, magharibi mwa Kenya.

After having a baby at and being forced to drop out of school at age 13, Evelina is finally able to resume her education. 

Evelina's story

Juni 22, 2017, Rais John Magufuli wa Tanzania alisema, “Ikiwa mimi ndie rais, hakuna mwanafunzi mwenye mimba atakaeruhusiwa kurudi shule.” Polisi na maafisa wa Tanzania pia wamewakamata wasichana wajawazito na kuzisumbua familia zao kuwataja wale waliowapa mimba. Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa ameitaja sera ya Tanzania ya “kushtusha,” wakati mwandishi maalumu wa tume ya Afrika ya haki za wanawake na Tume ya Wataalamu Afrika ya Haki na Ustawi wa Mtoto wameonesha kuguswa kwao na kusema serikali ya Tanzania haina budi kutimiza majukumu yake haki za binadamu.

Mwezi Mei 2018, Mahakama ya Haki ya Jumuiya ya Uchumi ya Mataifa ya Afrika Magharibi (ECOWAS) ilikubali kesi iliyoletwa dhidi ya serikali ya Sierra Leone kwa kukataa wasichana wajawazito kuhudhuria shule za umma.

201806WRD_Kenya_Pregnant_Girls_Education_phototn

A special interactive feature on empowering pregnant girls and adolescent mothers in to stay in school.

Read Now

Wasichana wanaopata mimba katika nchi nyingi za Afrika wanazuiwa kuendelea na elimu. Nchi nyingi pia hazina sera za kujiunga tena baada ya kujifungua. Baadhi ya nchi zenye kiwango kikubwa cha mimba za vijana kama vile Angola na Burkina Faso zinakosa sera za kusimamia ujauzito wa vijana shuleni.

Katika baadhi ya nchi, maafisa wa shule wanachukua hatua hatarishi za kugundua wasichana wajawazito, ikiwa ni pamoja na vipimo vya lazima vya mimba, na kuwanyanyapaa na kuwaaibisha hadharani au kuwafukuza. Vipimo hivyo bila ridhaa vinakandamiza haki yao ya faragha na heshima. Human Rights Watch waligundua kwamba wasichana wengine huogopa sana aibu hiyo na kupelekea kuacha shule kabla ya kugundulika pale tu wanapofahamu kuwa ni wajawazito. Wengine hufanya utoaji mimba usio salama, na kuweka maisha na afya zao katika hatari.

Nchi za kaskazini mwa Afrika kwa ujumla zinakosa sera zinazohusiana na namna ya kumhudumia msichana mjamzito shuleni. Wengine wanaweka faini na adhabu kali kwa wasichana na wanawake wanaoripotiwa kuwa na mahusiano ya kingono nje ya ndoa. Wasichana na wanawake wadogo wenye watoto, ambao huchukuliwa kama wanaleta aibu katika jamii zao, hudhihakiwa, kutengwa au hata kufungwa na hawatarajiwi kuwepo shule.

Kuna maendeleo ya dhahiri kwa nchi 26 za Afrika ambazo zina sheria au sera zinazolinda haki ya elimu kwa wasichana wajawazito kipindi cha ujauzito na uzazi, Human Rights Watch walisema. Nchi nne-ikiwa ni pamoja na Gabon na Côte d’Ivoire – zinawahakikishia wasichana haki ya kuendelea na shule kipindi cha ujauzito na baada ya kujifungua. Nyingine 22- ikiwa ni pamoja na Kenya na Malawi – zina zera za kujiunga tena zenye masharti. Benin, Cape Verde, na Senegali zimeondoa sera zinazotoa adhabu, na kupitisha sera zinazounga mkono wasichana kurudi shule. Hata hivyo, sheria na sera zinazohakikisha “kujiunga tena” mara kadhaa zinakosa usimamizi mzuri katika utekelezaji na hazisimamiwi vyema kuhakikisha shule zinazingatia.

Hata katika nchi zenye sera nzuri, wasichana hukabiliana na vikwazo kurudi shule. Shule nyingine zina masharti magumu kujiunga tena, zinazowavunja moyo wasichana kurudi. Kushinda vikwazo hivi, nchi nyingine-kama Gabon na Zambia – zimepitisha hatua za kumsaidia mama kijana kurudi shule, ikiwa ni pamoja na kuhakikisha hakuna ada kwa shule za msingi na sekondari, kuwapa muda wa kunyonyesha, kuwaruhusu wamama kuchagua kati ya zamu za kwenda shule asubuhi au jioni, na kuanzisha vituo vya kulea watoto karibu na shule.

Mwaka 2018, Umoja wa Afrika ulizitaka nchi wanachama “Kutokumuacha Nyuma Mtoto kwa Maendeleo ya Afrika." Umoja wa Afrika inabidi kuhakikisha kwamba wasichana wajawazito na kina mama vijana wanajumuishwa katika ajenda ya kutokumuacha nyuma mtoto, Human Rights Watch walisema.

Serikali hazina budi kupitisha kwa haraka sheria na sera zinazohimiza wasichana kuwepo shule, kurudi shule baada ya kujifungua, na kufaulu kitaaluma. Wote wanapaswa kuhakikisha kwamba hawaweki masharti makali kwa kina mama vijana ambao wanataka kuendelea na elimu.

Nchi zote hazina budi kupitisha mpango mkakati wa kusaidia kina mama vijana kuendelea na elimu, wakati wanapambana na sababu zinazopelekea mimba za mapema na zisizotarajiwa, Human Rights Watch walisema. Wanapaswa kuwapatia kina mama vijana huduma za kijinsia na afya ya uzazi, ikiwa ni pamoja na elimu inayojitosheleza kuhusu masuala ya ngono shuleni na katika jamii, na kuhakikisha upatikanaji wa njia mbalimbali za kujikinga na mimba, na njia salama na zinazokubalika kisheria za kutoa mimba.

“Kuwaadhibu wasichana wajawazito kwa kuwafukuza shule haimalizi mimba za utotoni,” alisema Martínez. “Nchi nyingi za Afrika zitashindwa kufikia malengo yao ya kutokumuacha mtoto nyuma kama watamtenga msichana mjamzito au alieolewa, lakini bara zima litafaidika pale wasichana wajawazito na kina mama vijana watakaporuhusiwa kuendelea na shule.”

Nukuu zilizochaguliwa

“Sikutaka kuwa na mtoto…nimewaeleza marafiki zangu wote wasijaribu kupata mtoto… inasababisha matatizo mengi … Lakini ikitokea umepata mtoto, basi lazima urudi shule baada ya kujifungua. Hakuna sababu ya kuona aibu. Kukosea ni ubinadamu.” – Fatoumata, 17, kutoka kusini mwa Senegali, aliepata mimba akiwa na miaka 16.

“Kule shule kulikuwa na muuguzi ambae alikuwa anatokea hospitali kuja kupima mimba. Walinipima na kugundua nina mimba. Walishika tumbo langu. Walifanya hivyo kwa wasichana wote kila mwezi. Kisha wakaandika barua kwa wazazi wangu kuwaambia kuwa nina mimba na walipaswa kufika shule. Walipofika walipewa barua kwamba nimefukuzwa shule. Nilikuwa na ujauzito wa miezi mitatu.” – Imani, 20, kutoka Mwanza, Tanzania, alipata mimba akiwa na miaka 16.

“Nilipata mimba nikiwa darasa la nane mwaka 2014. Nilihitaji pesa kujiandikisha kwa ajili ya mitihani yangu ya mwisho [ya kumaliza shule ya msingi]. Baba yangu alikuwa ameoa mke mwingine na kutuacha. Mama yangu hakuwa na pesa kabisa. Nilikutana na mwanaume aliekuwa akifanya kazi za muda kama mwalimu na kumueleza shida zangu. Alisema angenipa pesa. Nilianzisha mahusiano ya kingono naye, na hivyo ndivyo nilivyopata mimba. Jamii yangu inanikejeli. Wanafunzi wengine hawanitaki. Wananikejeli na kunicheka. Nilijiskia aibu kuwa mama katikati ya wasichana. Karibu niache shule, lakini Mkuu wa shule alinihimiza na mimi nikajipa moyo. Mama yangu alijitahidi kunisomesha, lakini sasa niko kidato cha tatu.” – Angela, 20, kutoka kata ya Migori magharibi mwa Kenya, aliepata ujauzito akiwa na miaka 16.

 

Your tax deductible gift can help stop human rights violations and save lives around the world.

Region / Country