Skip to main content

Kenya: Mahakama Yatupilia Mbali Mpango wa Kuwalazimisha Wakimbizi Kurudi Kambini.

Imekataa Mpango wa Kuwahamisha Wakimbizi 55,000 Wasomali na Wengine Walioko mijini.

Mnamo tarehe 26 Julai, 2013 mahakama kuu ya Kenya ilitupilia mbali mpango wa kuwahamisha wakimbizi 55,000 wengi wao wakiwa Wasomali kutoka mji mkuu wa Nairobi na miji mingine hadi kwenye kambi, shirika la kutetea haki za kibinadamu la Human Rights Watch lilisema leo. Mahakama ilisema kuwa uhamisho huu ungekiuka heshima ya wakimbizi, haki ya uhuru wa kutembea pamoja na kuwa kama kuwalazimisha kurudi Somalia ingawa sio kwa njia ya moja kwa moja. Kadhalika mahakama ilisema kwamba serikali haikuwa imethibitisha kwamba hatua hii ingesaidia katika kudumisha usalama wa kitaifa kufuatana na mashambulizi mengi ya mabomu na mengine nchini Kenya na watu wasiojulikana.

Kwa muda wa wiki 10 polisi waliwakiuka wakimbizi na wanaotafuta kimbilio kutoka Somalia na Uhabeshi kwa kuwatesa na kuwabaka – mwisho wa 2012 na mwanzo wa 2013. Polisi waliwaita wakimbizi “magaidi” na walisema kuwa wanapaswa kuhamia kambini.

“Uamuzi huu wa mahakama ulikaribishwa na unawapa nafuu wakimbizi 55,000 walioko mijini pamoja na kukumbusha kwamba Mamlaka hawayawezi kupuuza haki za wakimbizi,” alisema Gerry Simpson, mtafiti mwandamizi katika shirika la Human Rights Watch.

“Uamuzi huu wa korti unapaswa kutoa onyo kali kwa mamlaka kwamba dhuluma na vitisho dhidi ya wakimbizi walioko Nairobi vinapaswa kukoma.”

Serikali inapaswa kuwalinda wakimbizi, iruhusu Umoja wa Mataifa na makundi ya wakimbizi kuwapa msaada wakimbizi, na iwachunguze upesi maafisa wa polisi waliowakiuka vibaya zaidi wakimbizi katika mwaka wa 2012 na 2013, Human Rights Watch lilisema.

Mnamo Januari, shirika lisilo la kiserikali la Kituo cha Sheria liliipeleka mahakamani kesi hii iliyopinga uhalali wa mpango ule wa Disemba 2012 wa kuwahamisha wakimbizi. Chini ya mpango ule wakimbizi wote walioko mijini na wanaotafuta hifadhi walipaswa kuondoka kwenye miji ya Kenya na kurudi katika kambi zilizo chafu, zilizojaa kupita kiasi, na walimozuliwa kutembea kwa uhuru.

Mahakama Kuu ya Kenya iliamrisha mamlaka ziuhairishe mpango ule hadi itoe uamuzi wake. Mnamo tarehe 26 Julai mahakamu iliamua kwamba mpango ule ungekiuka haki nyingi za wakimbizi, kama vile haki ya kutembea kwa uhuru, haki ya kuheshimiwa, na ile ya uwezo wa kutorudishwa kwenye taabu, ambayo korti ilisema huenda ingetokea kwa kiwango kikubwa wakirudishwa kwa haraka kwenye kambi zilizochafu na zilizo mpakani mwa Kenya na Somalia.

Mnamo Januari tarehe 21, Human Rights Watch lilitoa witokwa mamlaka kuachana na mpango ule wao wa uhamisho, likisema kuwa Kenya imeshindwa kuthibitisha kulingana na sheria ya kimataifa kwamba mpango ule ulihitajika kama njia ya kuufikia usalama wa kitaifa au ni wenye vikwazo vya chini kabisa katika kushughulikia usalama wa kitaifa wa Kenya. Shirika la Human Rights Watch lilisema kuwa mpango ule aidha uliwabagua wakimbizi kinyume Na sheria kwa kuwa sera hii inawaruhusu Wakenya kutembea kwa uhuru ilhali inawanyima wakimbizi haki ile.

Human Rights Watch vilevile lilisema kwamba kuwahamisha maelfu ya wakimbizi kutoka mijini hadi kwenye kambi za wakimbizi ambamo hawawezi kutembea kwa uhuru zilizo pia na upungufu wa kifedha wa kiasi cha dola milioni 100 za Marekani, kungekiuka haki zao nyingine nyingi, ikiwemo haki ya kutembea kwa uhuru, haki ya kutofukuzwa kwa nguvu kutoka kwao, na haki ya kupunguziwa upatikanaji wa haki muhimu kama za chakula, kuchuma riziki, huduma ya afya, na elimu.

Maafisa walipokuwa wakitangaza hatua hii Desemba mwaka jana walisema kuwa hatua hii ingefuatwa mara moja na kurejeshwa Somalia, licha ya kuwa karibu maeneo yote ya Kusini hadi Kati bado ni hatari mno kwa sababu ya ghasia, mauaji, dhuluma za kiholela dhidi ya raia na mashirika yasiyo ya kiserikali yanayofikia eneo dogo.

Shirika la Human Rights Watch lilirudia wito wake kwa mamlaka za Kenya wa kutowashinikiza wakimbizi kurudi Somalia. Shinikizo hilo lingekiuka jukumu la Kenya la kutowarudisha kwa nguvu wakimbizi katika hali yenye mateso au dhuluma kwa jumla.

“Uamuzi huu unapaswa kuwa mwamko mpya kwa mamlaka kuhusu majukumu yao ya kimsingi kabisa kwa wakimbizi,” Simpson alisema. “Serikali haipaswi kutoa shinikizo wala kuwalazimisha wakimbizi kurudi katika sehemu zinazotishia maisha na uhuru wao.   

Your tax deductible gift can help stop human rights violations and save lives around the world.

Region / Country