- Serikali ya Tanzania imezidisha ukandamizaji wa kisiasa, Kuibua hatari na wasiwasi kwamba uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika tarehe 29 mwezi Oktoba 2025, hautakuwa huru na wa haki.
- Mamlaka zimedhoofisha upinzani wa kisiasa na ukosoaji wa Chama tawala, kuzuia uhuru vyombo vya habari, na kushindwa kuhakikisha tume ya uchaguzi inakuwa huru.
- Mamlaka zinatakiwa kuacha kuzuia sauti za upinzani na vyombo vya habari, na badala yake zishughulikie mabadiliko yenye maana kuhakikisha unafanyika uchaguzi huru na wa haki na wa kuaminika.
(Nairobi, Septemba 29,2025) - Serikali ya Tanzania, imezidisha ukandamizaji wa kisiasa, ikiibua hatari ya wasiwasi kwamba uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika tarehe 29, mwezi, 2025 hautakuwa wa huru na haki. Shirika la kuangalia haki za binadamu linesema leo, mamlaka zimekandamiza upinzani wa kisiasa na ukosoaji wa Chama tawala, kuzuia uhuru wa vyombo vya habari, na kushindwa kuhakikisha kwamba tume ya uchaguzi inakuwa huru.
“Mamlaka za Tanzania zinatakiwa kuchukua hatua za haraka ili kulinda uadilifu wa uchaguzi wa mwezi Oktoba, ambao uko katika hatari kubwa", alisema Nomathamsanqa Masiko-Mpaka mtafiti wa Afrika katika shirika la Kusimamia haki za binadamu,” mamlaka zinahitaji kuacha kuzuia sauti za upinzani na vyombo vya Habari na badala yake zishughuĺikie mabadiliko yenye maana kuhakikisha uchaguzi huru wa haki na wenye kuaminika unafanyika."
Kutoka mwezi wa Julai mpaka mwezi wa Septemba 2025, shirika la kusimamia haki za binadamu liliwahoji watu kwa njia ya mtandao au ana kwa ana na wanaharakati wa mashirika ya kiraia wanasheria, viongozi wa dini, wanataaluma, waandishi wa Habari na wanachama wa chama cha upinzani, ikijumuisha na waathirika wanane waukatili, kutoka Tanzania bara na Zanzibar. Shirika la kusimamia haki za binadamu lililiandikia jeshi la polisi, tume huru ya Taifa ya uchaguzi, mamlaka ya kudhiti mawasiliano na wizara ya mambo ya nje tarehe 19/Septemba kuwasilisha utafiti na kuomba taarifa juu
ya tuhuma, lakini halijapata jibu lolote hata mpaka wakati wa uchapishaji.
“Haki ya kuishi kwa watu ambao wana maoni tofauti toka serikalini imo hatarini", Kiongozi wa dini ambaye alisema kuwa alishambuliwa kwa uanaharakati, alililiambia shirika la kusimamia haki za binadamu. "Watu wanatakiwa kuikosoa serikali. Haitakiwi kuhatarisha maisha yao. Utekaji, utowekaji na baadhi ya muaji ya watu ambayo hayawezi kuelezeka. Na huwezi kupata maelezo kutoka serekalini.”
Shirika la Human Rights Watch lilirekodi visa 10 vya mashambulio, unyanyasaji, utekaji nyara na mateso vilivyokuwa na misukumo ya kisiasa, na pia likaonyesha jinsi vizuizi vingi vilivyoathiri vyombo vya habari vya kawaida na mitandao ya kijamii.
Katika tukio moja lililotokea tarehe 2 mwezi Mei, watu wasiojulikana walimpiga na kumteka nyara mwana harakati maarufu wa chama cha upinzani mpaluka Nyagali, almaarufu kama mdude, toka katika makao yake huko Mbeya kusini Magharibi mwa Tanzania, mke wake aliviambia vyombo vya habari. Mahakama kuu ya Mbeya ilipuuzia agizo la mke wake la kufikishwa mahakamani tarehe 9 mwezi Julai, na alipelekwa mdude hapakufahamika. Polisi walikana kuhusika na utekaji nyara wake.
Tarehe 16 mwezi Juni, katika Dar es salaam, wavamizi wasiojulikana walimpiga Japhet Matarra, mkosoaji wa mara kwa mara wa serekali katika mtandao wa X (ambao hapo Zaman ulijulikana kama Twitter, alipigwa na kipande cha chuma mpaka akapoteza famamu. Ambapo ilibidi asubiri upasuaji hospitalini, ghafla watu waliovaa kama madaktari waliingia chumbani mwake na kumshambulia. Aliwapigia kelele na wakakimbia. Picha zimeonwa na shirika la kusimamia haki za binadamu. Alionyesha majeraha yake ya taya la chini, na zaidi ya mwezi baada ya shambulio lao, bado ilikuwa ni vigumu kwake kuzungumza.
Utafiti wa Shirika la Human Rights Watch ulithibitisha matokeo ya mashirika ya haki za binadamu nchini Tanzania. Kituo cha sheria na haki za binadamu( The Legal and Human Rights Center) kilirekodi takriban visa 100 vya utekaji nyara na kupoteza watu kwa nguvu kati ya mwaka 2015 na Februari 2025. Muungano wa walinzi wa haki za binadamu Tanzania ulirecordi mashambulizi 48 kwa walinzi wa haki, wanaharakati na watu wengine katika mwaka 2024.
Katika mwezi Juni polisi walitoa majibu kwa kiasi kikubwa cha watu wanaopotea kwa kutoa orodha ya maelezo kwa wale ambao walituhumiwa kuandaa utekaji. Orodha haikuhusisha kesi maarufu za wapinzani na wanachama wa mashirika ya kiraia, ikilazimisha maswala yanyohusu uaminifu na uadirifu ya tafiti za serikali.
Serikali pia ilikandamiza vyama vya upinzani na wanachama wake. Katika mwezi wa Aprili, mamlaka zilimkamata tundu lissu, kiongozi wa Chama kikuu Chama Cha Demokrasia na maendeleo (Chadema), wakati wa maandamano ya mkutano wa kampeni. Amekuwa akikabiliwa na kesi ya mashitaka yaliyotengenezwa, Pamoja na uhaini ambayo haina dhamana na ambayo inabeba adhabu ya kifo. Akihudhuria kesi ya Lissu mmoja wa mtumishi wenza alisema, “katika vipindi vingi, na hasa ninapokwenda kuhudhuria mashauri ya mwenyekiti wetu wa Taifa nanyanyaswa-wananizuia hata nisifike kwenye majengo ya mahakama, na wananipiga.”
Mpinzani mwingine alisema; “Sijisikii salama kuwa mwana siasa katika nchi ya Tanzania. Sijisikii huru kuikosoa serikali.... Tunajikuta katika mashambulizi sugu ya polisi.”
Tume huru ya Taifa ya uchaguzi (INEC) ambayo, mbali na jina lake inachaguliwa na raisi na ambayo maamuzi yake hayawezi kutolewa changamoto zake mahakamani, ilizuia Chadema kushiriki uchaguzi kwa kutokukubali kusaini kanuni za maadili. Katika mwezi wa Juni koti kuu ilisimamisha shughuli za Chama cha Chadema kabisa kwa sababu ya mabishano ambayo ni tofauti kabisa. Tangu wakati huo tume ye uchaguzi imezuia uteuzi wa Luhaga Mpina mgombea wa uraisi wa Chama cha ushirika wa mabadiliko na uawazi (ACT-Wazalendo).
Serikali ya Tanzania ya raisi Samia Suluhu Hassan imeahidi katika baraza la haki za binadamu la umoja wa Mataifa mwezi Juni kutetea haki za binadamu na misingi ya haki za Kidemokrasia kwa kipindi chote cha uchaguzi. Hata hivyo tangu wakati huo,serikali bado haijafanya mabadiliko yanayohitajika.
Tume ya uchaguzi kupiga marufuku vyama vya kisiasa vya upinzani na wagombea uraisi wa vyama vya upinzani wanaondoa kabisa ushindani unaokikabili Chama Cha Mapinduzi, lilisema shirika linalosimamia haki za binadamu. Serikali imeendelea na ukaguzi wake mkali kwenye vyombo vya habari kuelekea kwenye uchaguzi, ikizuia haki ya uhuru wa kujieleza na kutoa taarifa, na kushinikiza matokeo ya kupumzika kwenye chombo cha habari.
Katika miezi ya hivi karibuni, kamati ya Afrika ya binadamu na haki za watu (African Commission on Human and People’s Rights), Wataalamu wa haki za binadamu wa umoja wa mataifa (United Nations), na bunge la umoja wa ulaya (European Parliament), wameibua hoja kuhusu mazingira ya uchaguzi katika Tanzania. Taasisi zilinukuu ukandamizaji wa mikutano ya hadhara na mikusanyiko ya amani,kutoweka kwa lazima kwa watu,mateso na kukamatwa isivyo harari,kuzuia haki ya kupata habari, na uhuru wa vyombo vya habari na kuongea,ukijumuisha kuzuiwa kupata tovuti za habari kwa kiswahili.Kufutwa utoshiriki na tume huru ya uchaguzi ya wagombea uraisi na vyama vya siasa kumeibua
Maswali kwamba kila uchaguzi wa Tanzania hautakuwa unaakisi matakwa ya wapiga kura,” Masiko-Mpaka alisema. “Serikali inahitaji kwa haraka sana kuacha kuukandamiza upinzani wa kisiasa,bila upendeleo kuchunguza mashambulio na utekaji nyara wa wanaharakati wa haki za binadamu, wanachama wa upinzani,wanasheria na viongozi wa dini, na kuhakikisha kuwa kunakuwepo na tume huru ya uchaguzi.”
Kwa maelezo zaidi yanayohusu maswala ya haki za binadamu tukielekea kwenye uchaguzi wa Oktoba,tafadhali angalia hapa chini.
Unyanyasaji, Ushambuliaji, Utekaji nyara na mateso mengineyo.
Shirika la Human Rights Watch lilirekodi kesi 10 ambazo mamlaka za Tanzania zliinyanyasa, zilishambulia, ziliteka nyara na kuwateka wanaharakati wa haki za binadamu, wanachama wa vyama vya upinzani, wanasheria na viongozi wa dini tangu katikati ya mwaka 2024.
Tare 23 mwezi Juni 2024, katika jiji la Dar es salaam wanaume ambao walikuwa askari polisi walimkamata Edgar Mwakabela isivyo halali, mwanaharakati aliyefahamika, ambaye alisema kuhusu kunywea kwa demokrasia na nafasi ya kisiasa nchini. Walimchukua hadi kituo cha polisi ambapo walimvua nguo zake, wakampiga na fimbo za chuma na wakamnyima chakula, maji na kutokumwonyesha mahali pa kwenda chooni. Siku iliyofuata walimhamishia kituo cha polisi cha Arusha, kaskazini mwa Tanzania na wakaendelea kumshikiria hapo kwa siku tatu. Tarehe 26 mwezi Juni walimbeba ndani ya gari wakaendesha kwa masaa matatu hadi manne halafu wakampiga na kumwacha akiwa hajitambui, katika mbuga ya wanyama ya katavi, karibia kilometa 1,300 kutoka Dar es salaam.
Vyombo vya habari vilitoa taarifa kwamba tarehe 6 mwezi Septemba, 2024, wanaume wasiojulikana wenye silaha walimteka nyara Ali Kibao aliyekuwa mwana Chama mstaafu na aliyekuwa afisa wa jeshi mstaafu kitengo cha upelelezi, akiwa Dar es salaam baada ya land cruiser mbili nyeupe kulizuia basi ambalo alikuwa akisafiria. Mwili wake ulipatikana siku moja baadaye katika viunga vya jiji la Dar es salaam. Mwenyekiti wa chadema wa wakati huo aliviambia vyombo vya habari kwamba baada ya upasuaji wa mwili wake ulionyesha kwamba kibao alikuwa amepigwa vibaya sana na mwili wake kumwagiwa tindikali. Wakati raisi Samia alipotoa taarifa hii aliagiza uchunguzi ufanyike juu ya jambo hili. Hakujawakuwepo ukamataji wa wahusika juu ya swala hili.
Vyanzo vya kuaminika vilisema kwamba tarehe 12 mwezi Januari 2025, Maria Sarungi Tsehai mmiliki maarufu wa vyombo vya habari na mkosoaji wa raisi Hassan, alitekwa nyara huko Nairobi, Kenya. Alifunikwa macho, akafungwa pingu, hakuweza kuwaona watekaji wake ambao waliendelea kumwomba namba za siri za simu zake. Wakati wa mkutano wa kupashana habari baada ya kuachiwa kwake, Sarungi alisema, “Nina hakika kwamba sababu ya utekaji nyara ilikuwa ni kupata mitandao yangu ya kijamii [kwa sababu] ya kufichua udandanganyifu wa kazi niyoifanya.
Tarehe 20 Juni, mwenyekiti wa tawi la wanawake la ACT wazalendo, Janeth Rithe alijisalimisha kwa polisi baada ya wao kuja makao makuu ya Chama Dar es salaam wakimtafuta.Mwana Chama wa ACT wazalendo na taarifa za vyombo vya habari zilionyesha alikuwa amekamatwa kwa kusema wakati wa mkutano wa kampeni kwamba raisi alikosea kuhusu hali ya uchumi wa Tanzania na chama tawala kilikuwa kinaendesha jeshi la polisi. Jeshi la polisi lilimshikilia zaidi ya saa 24 halafu likamwachia tarehe 23 Juni, bila kufunguliwa mashitaka.
Viongozi wa kidini wamekabiliwa na mashambulio baada kusema ukweli. Usiku wa tarehe 30 Aprili, mshambuliaji asiyejulikana alimpika kwenye kichwa Padre Charles Kitima, Padre mashuhuri wa romani katoliki na mkosoaji wa serikali, katika kituo cha mikutano Dar es salaam. Mashambulizi yalitokea muda mfupi baada ya video kusambaa ambayo aliitolea wito mabadiliko kabla ya chaguzi.Alilitolea tukio hilo taarifa polisi lakini hakuna aliyekamatwa.
Katika mwezi Juni, Serikali iliondoa usajiri wa moja ya makanisa makubwa ya Pentecost nchini baada ya baada ya mwanzilishi wake, Askofu Josphat Gwajima, mbunge wa chama tawala Chama cha mapinduzi CCM kuzungumza dhidi ya utekaji nyara unaoongezeka na ukiukwaji wa haki nyingine za binadamu. Wizara ya mambo ya ndani ilisema haya maoni yalitafuta kukosanisha serikali na raia wake. Mwanaharakati wa haki za binadamu alisema: “Askofu Gwajima kutoka cha CCM alisema wazi kwamba yuko kinyume na utekaji na makanisa yote ambayo yanamhusu yamefungwa mpaka sasa.”
Mwanasheria alisema kwamba alipona majaribio matatu ya utekaji nyara, pamoja na mwili mwaka 2024. Wakati wa jaribio la hivi karibuni mwezi Desemba, wanaume wawili ambao walikuwa wamevaa kiraia na bila vitambulisho walimfuata wakati alipokuwa ameegesha gari ofisini kwake na wakajitambulisha kama maaskari polisi. Alikimbia kwa miguu lakini wanaume hao wawili walichukua laptop pamoja na hati kutoka ofisini mwake. Alisema kwamba alikuwa amelengwa kwa sababu aliibua kesi dhidi ya serikali.
Vyanzo vya kukubalika vilisema polisi walipitia picha za CCTV na wakathibitisha kwamba watu waliomfuata walikuwa ni maaskari polisi lakini wakadai kwamba lilikuwa ni swala la utambuzi usio sahihi. Wakati wa jaribio la utekaji mapema mwaka 2024, maaskari polisi pia wakadai swala la kukosewa kwa utambuzi.
Kukosekana kwa uhuru wa tume ya Taifa ya uchaguzi
Katika mwezi wa Aprili, tume huru ya Taifa ya uchaguzi ilipiga marufuku Chadema kutotoa wagombea katika uchaguzi unaokuja na katika chaguzi ndogo mpaka mwaka 2030, kuimarisha uhusiano kuhusu uhuru wa tume. Tume ilikipiga marufuku Chama kwa sababu ya kukataa kwake kusaini kanuni za maadili za Aprili 12,2025, Ingawa sheria inayotambulika, sheria ya Taifa ya uchaguzi haichambui ili kuelezea ratiba.
Uamuzi wa tume kufuta ACT Wazalendo kushiriki uchaguzi wa wa mgombea uraisi, Luhaga Mpina, uliongeza wasiwasi zaidi. Luhaga Mpina alikuwa ameshatumikia serikali kama waziri wa serikali hapo awali chini ya raisi John Pombe Magufuli. Uamuzi wa tume ya uchaguzi ukifuatiwa na wa msajiri wa vyama vya siasa ulitoa maamuzi kwamba uteuzi wa Mpina ulikiuka taratibu za ndani za Chama cha ACT-Wazalendo. Mnamo tarehe 11 Septemba, mahakama kuu ilitoa mwongozo kwamba chini ya katiba, tume hailazimishwi kukubali maelekezo kutoka kwenye mamlaka husika, na lazima ikubali fomu ya uteuzi wa Mpina. Wakati tume ikifanya hivyo tarehe 13 mwezi Septemba, siku mbili baadaye, ilitangaza kwamba ilikuwa imemfuta Luhaga Mpina kufuatia pingamizi kutoka kwa mwanasheria mkuu.
Wajibu wa muda mrefu wa tume huru ya uchaguzi unaibuka kutoka kifungu cha 74 cha katiba ya Tanzania, ambacho kinampa mamlaka raisi kuteua, kufukuza wanachama wa tume ikijumuisha mwenyekiti na makamu mwenyekiti. Mahakama ya Afrika inayohusu binadamu na haki zao(ACHPR) na waigizaji wengine imeibua wasiwasi kwamba mahakama haziwezi kuzingatia kesi ambazo zinaleta changamoto kwenye uamuzi wa tume chini ya kifungu cha 74. Katika mwezi Februari mwaka 2024, bunge lilipitisha seti ya sheria kugeuza mfumo ambao unatawala chaguzi. Hata hivyo haya hayakuhusu teuzi za wanachama wa tume na mahakama za ndani kukosa haki juu ya tume na kutoa changamoto kwenye uamuzi wa tume chini ya kifungu cha 74. Katika mwezi Februari mwaka 2024 bunge lilipitisha seti ya sheria kugeuza mfumo unaotawala uchaguzi. Hata hivyo haya hayakuzungumzia teuzi za raisi za wanachama wa tume na mahakama za ndani na ukosefu wa haki juu ya kamati za maamuzi.
Makatazo ya kutokupiga kura Zanzibar.
Watumishi na wanaharakati wa upinzani walisema kwamba maelfu ya wapiga kura Zanzibar, kisiwa ambacho ni nusu huru hawakuweza kupata vitambulisho vyao ambavyo vinahitajika kwa kujisajili kupiga kura. Vitambulisho ni vya muhimu ili kupata huduma nyingi za serikali, pamoja na kujisajil i kupiga kura. Hata hao waliofanikiwa kujisajili wanahangaika kupata vitambulisho vyao kwa sababu mamlaka zinawahitaji watu kuvichukua kutoka ofisi za wilaya, ambapo hapo awali vilipatikana katika maeneo yao. Mtetezi wa haki za binadamu alisema: "[k ]ama mfumo ukikudhania kuwa unapiga kura upande wa upinzani hupati kitambulisho cha mzanzibari. Unahitaji mtu katika serikali za mitaa kukupitisha kama mkazi katika eneo hilo. Mtumishi wa serikali za mitaa katika eneo hilo awe anakujua vizuri sana na awe anajua wapi ulikotokea. Kama ni familia ambayo kwa kawaida inapigia kura upinzani basi hataweza kukipata".
Vizuizi vya vyombo vya habari
Mamlaka za Tanzania zinazuia vyombo vya habari kwa ukali. Sheria ya uharibifu wa mtandaoni ya mwaka 2015, Sheria inayohusu umeme na mawasiliano ya posta ya 2022, na mambo ya umeme na mawasiliano ya posta (maudhui ya mtandao) kanuni ya mwaka 2020 unaipa mlamlaka ya Urekebishaji wa mawasiliano Tanzania((TCRA) kwa busara kubwa inasimamisha matumizi ya vyombo vya habari ambavyo vinatumia taarifa zenye utata kama vile " udandanganyifu, Upotoshaji na nyingine zisizo sahihi.
Katika mwezi Oktoba 2024, mamlaka ya mawasiliano ilisitisha leseni za mtandao za magazeti matatu ambayo yanaongoza – the Citizen, Mwananchi, na Mwanaspoti – kwa siku 30 baada ya kueneza clip yenye michoro katika utekaji nyara ulioongezeka nchini.
Katika mwezi wa mei, mamlaka iliifungia zaidi ya mitandao 80,000 akaunti za mitandao ya kijamii, blogs na majukwaa ya mtandao yaliyokuwa yakichapisha maudhui ambayo hayakuwa na maadili ambayo yalikuwa na hatari kwa afya ya akili ya watoto.
Tangu mwezi mei serikali imezuia kupata mtandao wa X ikidai kuwa kituo kinaonyesha mudhui ya picha zenye kutia ashiki. Mamlaka pia zilizua kupata programu ya kusikiliza ya kijamii na huduma ya mawasiliano ya kutumiana jumbe za telegramu.
Mnamo Septemba 6 mamlaka ya mawasiliano isitisha mtandao wa JamiiForums, jukwaa la mtandao la kitanzania ambalo hurahisisha mazungumzo na kufichua maovu kwa siku 90. Mamlaka ilisema jukwaa hilo lilikuwa limechapisha maudhui ambayo yalipotosha umma, lilitukana na liliidharau serikali na raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.”
Mmiliki mmoja wa vyombo vya habari alisema kuwa walikuwa wamepokea barua kadhaa kutoka kwenye mamlaka ya urekebishaji ikidai kwamba wahariri maudhui.
Mwandishi wa habari ambaye aliambiwa mara mbili na mamlaka za mawasiliano kuondoa maudhui, ikijumuisha na makala kuhusu familia ambazo Jamaa zao wametekwa nyara zilisema: “kama mrekebishaji akikwambia uandike maudhui fulani unaweza kufanya hivyo kuepuka hatari inayoweza kukutokea. Unaweza kufutiwa leseni au tovuti kuondolewa kwenye mtandao na watu hawataweza kukupata tena.”
Mmiliki wa mtandao ambaye aliikimbia Tanzania alisema alikwishapokea vitisho vya kuuwawa kwa ajili ya jukwaa la vyombo vya habari ambako anafanya kazi. “Najua kuna athari na ndiyo maana ilinilazimu kukimbia.” Hawajui nilipo.... Nimeambiwa nibaki salama popote nilipo hata na watu kutoka kwenye Chama tawala.” Aliripoti kwenye mamlaka na zimeipigia simu familia yake mara kadhaa wakiuliza mahali alipo.
Chanzo, chombo cha habari cha kidigitali katika Tanzania ambacho kinatoa uandishi huru kwa manufaa ya wananchi kilitoa maelezo yakisema kilikuwa kikiandika makala kuhusu tarehe 24 Mei zikiwa ni habari za mkutano kuhusu utekaji nyara katika Tanzania zikimhusisha Askofu Gwajima baada ya mamlaka ya mawasiliano kutoa mwongozo.
Mwandishi wa habari mmoja alisema kwamba mamlaka ziliviita vyombo vya habari isivyo rasmi, kujuisha na chake, ili kuahirisha mkutano wa utoaji habari wa askofu: “Watu wengi waliishusha hadhi hatua hiyo lakini sisi hatukufanya hivyo,” alisema. “Tuliposhindwa kufanya hivyo walikwenda kwenye bodi ya urekebishaji [TCRA]. [Watu kutoka ikulu] wakati mwingine wanatoka ofisi ya raisi. Najua wanatoka kwenye ofisi ya raisi kwa sababu wanafanya kazi humo TCRA ni mbwa mkubwa wa hatari mbwa wa kufugwa ambao wangeweza kufunguliwa mnyororo kukufuata”
“Kama tunataka kuwa waaminifu,” alisema mwandishi mmoja wa habari. “Hakuna uhuru kwa ajili ya uandishi wa habari wa kujitegemea.”