Skip to main content

Ziara ya Tanzania Hatarini Kusafisha Uondoshwaji wa Nguvu wa Maasai

Utalii Unapaswa Kuheshimu Haki za Jamii Wenyeji

Patrick McEnroe (left) and John McEnroe Jr. arrive on court for the opening of the Laver Cup tennis event, London, September 23, 2022. © 2022 Peter van den Berg/USA TODAY Sports/Reuters

Wiki hii wacheza tenesi kutoka Marekani – wanandugu John na Patrick McEnroe – wanajiandaa kuwa wenyeji wa ziara ya kitalii yenye maudhui ya mchezo wa tenesi katika eneo la Hifadhi ya Ngorongoro ambapo wenyeji wa eneo hilo ambao ni Maasai wanapinga vitendo vya Serikali ya Tanzania kuwaondoa kwa nguvu katika maeneo yao ya asili

Ziara ya Kitalii ijulikanayo kama “Epic Tanzania Tour” inaandaliwa na kampuni binafsi ya usafirishaji, Insider Expedition na serikali ya Tanzania. Rais Samia Suluhu Hassan ameidhinisha ziara hiyo. Kwa mujibu wa ratiba ya ziara hiyo, watalii watatembelea “Kijiji cha Utamaduni wa Maasai,” wakati wanandugu McEnroe wakitoa mafunzo ya tenesi kwa watoto wa Kimaasai.

Kwa miongo kadhaa sasa, serikali imetumia wasiwasi wa ongezeko la idadi ya watu na mifugo kuhalalisha kuzuia jamii za wafugaji wa Kimaasai–wengi wao wanategemea ufugaji kuendesha maisha yao – kuishi na kuchunga mifugo yao katika maeneo ya hifadhi ya Ngorongoro ikiwa ni pamoja na ndani ya bonde la Ngorongoro.

Tofauti na Wamaasai ambao wamekuwa wakiishi hapo kwa miongo kadhaa, wacheza tenesi na watalii wataruhusiwa kufika bonde la Ngorongoro (kreta), bonde kubwa zaidi duniani lililotokana na volcano.

Mnamo mwaka 2021, serikali iliweka mpango, bila ya kuwashirikisha ipasavyo jamii ya Wamaasai, kuwahamisha kwa “hiari” wakazi wote 82,000 na kuwapeleka eneo lililopo takribani umbali wa kilometa 600 katika wilaya ya Handeni iliyopo mashariki mwa Tanzania kufikia 2027. Katika kuhakikisha wanaondoka, serikali ilipunguza huduma muhimu za afya na elimu na kupunguza bajeti ya Halmashauri ya Ngorongoro ambayo inachangia huduma muhimu za kijamii kwa jamii iliyopo pale.


Mamlaka pia imechukua hatua kuzuia wakazi, ambao wanategemea ufugaji kuacha kufuga mifugo na kuzuia mifugo yao kufikia maeneo muhimu ya vyanzo vya maji. Maafisa Wanyamapori walioajiriwa na serikali mara kwa mara wamekuwa wakiwapiga na kuwakamata wanajamii kwa kuingiza mifugo yao kreta na maeneo mengine yaliyozuiwa. Tangu Februari 2022, serikali imeweka vizuizi, kuwalazimisha wakazi kuonyesha vitambulisho kuthibitisha kuwa wanaishi kwenye eneo la Hifadhi ya Ngorongoro kabla ya kuruhusiwa kuingia.

Wiki hii, Human Rights Watch iliandika kwa Insider Expeditions na wanandugu McEnroe kuwajulisha juu ya uvunjifu wa haki na kuwaomba kuongea hadharani kupinga vitendo vya uvunjifu wa haki za binadamu uliofanywa na serikali ya Tanzania maeneo hayo lakini haijapokea majibu.

Wanaharakati wa Tanzania wamekosoa ziara hiyo. Edward Porokwa, mkurugenzi wa taasisi isiyo ya kiserikali ya Pastoralists Indigenous Non Governmental Organization’s Forum au Pingo’s Forum iliyopo Arusha anaielezea “The Epic Tanzania Tour” kama ziara “isiyowajibika,” na kusema inaonyesha “namna utalii usivyojali kuhusu haki za binadamu.”

Ziara hii ya ‘The Epic Tanzania Tour’ inahatarisha kukejeli masaibu yanayokabili jamii za wafugaji wa Kimaasai ambao walikuwa wakiishi katika maeneo ya Hifadhi ya Ngorongoro na kutumia michezo kusafisha tuhuma dhidi ya serikali juu ya uvunjifu wa haki za binadamu katika eneo hilo. Utalii haupaswi kufanyika kwa gharama za jamii ya wenyeji ambao wanaondolewa kwa lazima kwa kutumia mwavuli wa uhifadhi.

Wachezaji tenesi ambao watashiriki katika ziara hii hawana budi kutumia jukwaa hilo kuitaka serikali ya Tanzania kuzingatia haki za binadamu katika eneo hilo badala ya kupuuza.Your tax deductible gift can help stop human rights violations and save lives around the world.

Region / Country