Kesi isiyo ya kawaida itaanza kusikilizwa wiki ijayo katika mahakama kuu ya London: famila za wanaume wawili wa kitanzania wenye umri wa miaka 23 walipigwa risasi na kufariki mwaka 2019 katika mgodi wa dhahabu unaoendeshwa na kampuni ya Canada Kaskazini mwa Tanzania, wanafungua kesi dhidi ya chama cha soko la dhahabu la London (LMBA),ambacho ni chombo cha sekta kinachosimamia soko la dhahabu la London.
Watanzania wengine 30 walijiunga hivi karibuni na kesi hiyo baada ya mahakama nchini Canada kufuta kesi nyingine kuhusu mauaji kwa kusema haina mamlaka. Familia zinatafuta fidia, kwa uamuzi wa LBMA wa kupata cheti cha dhahabu kutoka kwenye mgodi huo kikithibitisha kuwa ni “dhahabu inayozingatia uwajibikaji”.
Vikundi vya haki za binadamu vimeripoti kwa miaka mingi kwamba polisiwamewaua na kuwajeruhi watu waliokosa kwa kuingia bila ruhusa na kuchimba madini katika mgodi wa Mara Kaskazini. Barrick gold mmliki wa mgodi amethibitisha kwamba vifo vilitokea, lakini amesema kwamba polisi hawakuwa chini ya mamlaka yake.
Licha ya vifo vilivyotokea katika eneo hilo kiwanda cha kusafisha dhahabu cha India kilichopo Uswisi kiliendelea kununua dhahabu kutoka kwenye mgodi huo hadi mwaka 2024. Kama mwanachama wa LBMA, kiwanda hicho kilikaguliwa kila mwaka ili kuangalia uzingatiaji wa "Miongozo ya uwajibikaji kwenye dhahabu" ya LBMA-kiwango kinachotaka makampuni kutambua na kufanyia kazi vihatarishi vya haki za binadamu katika mnyororo wao wa usambazaji. Famlia za waathirika wanadai kwamba LBMA ilithibitisha kwa makosa dhahabu kutoka Mara Kaskazini. LBMA inasema haikubali kuwa "vifo vya kusikitisha vilisabishwa au vina uhusiano na kazi, wajibu au majukumu ya LBMA". Kiwanda hicho kilisema kilifuata kwa umakini miongozo ya LBMA ya uwajibikaji kwenye dhahabu.
Kesi inaashiria tatizo kubwa zaidi. Mfumo wa udhibitishaji wa viwanda mara nyingi hutegemea ukaguzi wa juu juu na usio na uwazi. Uchunguzi wa shirika la haki za binadamu(HRW) uliofanyika mwaka 2023 uligundua kwamba LBMA ilithibitisha kwamba dhahabu kutoka mgodi wa Ethiopia kwamba, "umezingatia uwajibikaji" hadi mwaka 2018 licha ya unyanyasaji mkubwa wa haki, ikiwa ni pamoja na uchafuzi mbaya wa mazingira na athari za kiafya kwa watoto na wanawake wajawazito. LBMA ilijibu kwamba miongozo iliyokuwa ikitekelezwa kwa wakati huo haikujumuisha athari za mazingira.
Ingawa LBMA hivi karibuni ilichukua hatua kuelekea kwenye uwazi zaidi-ikihitaji kufichua wasambazaji maeneo nyeti yenye "alama nyekundu"-sheria thabiti zaidi zinahitajika. Serikali zinapaswa kupitisha sheria zinazoyataka makampuni kuheshimu haki katika minyororo yao ya usambazaji duniani. Vyombo vya usambazaji vinapaswa kuboresha sana ukaguzi wao, kuchapisha ripoti za ukaguzi, na kuwataka wanachama wao kuweka wazi minyororo yao ya usambazaji.
Wakati huo huo kesi hii inaweza kuthibitisha kuwa ni muhimu kwa familia zinazotafuta haki- na kwa mienendo ya sekta ya dhahabu.