“Adila K.,” 35, alisema alirudi kutoka Oman mwezi Januari 2017 baada ya kukaa mwaka mmoja akifanya kazi katika familia moja ambayo walitaifisha hati yake ya kusafiria, walimlipa pungufu ya alichoahidiwa, na alilazimishwa kufanya kazi kwa masaa mengi bila kupumzika au kuwa na siku ya mapumziko. Kijiji cha Kiwangwa, Tanzania
© 2017 Rothna Begum/Human Rights Watch
Mwajuma H., 27, alisema mwaka 2015 alikimbilia ubalozi wa Tanzania nchini Oman baada ya mwajiri wake kumnyanyasa kimwili na kutokumlipa mshahara. Ubalozi ulikubali wakala wake amchukua kwa makubaliano kwamba watamrudisha nyumbani licha ya Mwajuma kulalamika kwamba wakala huyo hupiga wanawake. Wakala alimlazimisha kufanya kazi na mwajiri mpya bila malipo. Dar es Salaam, Tanzania.
© 2017 Rothna Begum/Human Rights Watch
Lulu Omar, mratibu wa watumishi wa ndani Zanzibar: Chama cha Wafanyakazi wa Ndani, Mahotelini na Uhifadhi wa Tanzania (CHODAWU-Z), akielezea kampeni yake ya kusajili watumishi wa ndani wa Kitanzania kabla ya kuhama. Stone Town, Zanzibar, Tanzania.
© 2016 Rothna Begum/Human Rights Watch
Baadhi ya wanawake ambao wanapata fedha za kutosha wanaweza kujenga nyumba kwa ajili yao na familia zao. Wanawake wengi wanahama wakiwa na ndoto za kuweza kujenga nyumba kwa ajili ya familia zao. Ujenzi wa nyumba, Majohe, Dar es Salaam, Tanzania.
© 2017 Rothna Begum/Human Rights Watch
Watumishi wa ndani wakiwa katika semina huko Zanzibar mwezi Oktoba 2016, wakijadili njia za kushirikiana na kusaidia haki za watumishi wa ndani wa Kitanzania katika nchi za Ghuba. Zanzibar, Tanzania.
© 2016 Rothna Begum/Human Rights Watch
Bango linaloelezea haki za mtumishi wa ndani katika ofisi huko Zanzibar: Chama cha Wafanyakazi wa Ndani, Mahotelini na Uhifadhi wa Tanzania (CHODAWU-Z). Stone Town, Zanzibar, Tanzania.
© 2016 Rothna Begum/Human Rights Watch
Hati ya kusafiria ya mtumishi wa ndani wa zamani wa Kitanzania ikiwa na viza ya ajira ya Oman. Dar es Salaam, Tanzania.
© 2017 Rothna Begum/Human Rights Watch
Dotto B., 32, alisema mwajiri wake Oman alimyanyasa kimwili, alimlazimisha kufanya kazi kwa saa 20 kwa siku bila mapumziko wala siku ya mapumziko, na alimlipa Riyali 50 ($130) badala ya Riyali 80 ($208) kwa mwezi kama ilivyo kwenye mkataba. Mwanza, Tanzania.
© 2017 Rothna Begum/Human Rights Watch
Deograsia Vuluwa, Mkurugenzi wa Jinsia, Wanawake na Watoto katika Chama cha Wafanyakazi wa Ndani, Mahotelini na Uhifadhi wa Tanzania (CHODAWU), mtetezi anaehimiza Tanzania kutoa ulinzi bora kwa watumishi wa ndani wa Kitanzania wanaofanya kazi Mashariki ya Kati. CHODAWU pia inafanya kampeni ya Tanzania kupitisha Mkataba wa ILO wa Watumishi wa Ndani. Dar es Salaam, Tanzania.
© 2017 Rothna Begum/Human Rights Watch
Cecilia, 22, alisema akiwa Oman alikuwa akifanya kazi kwa saa 16 kwa siku bila mapumziko wala siku ya mapumziko, na alikuwa akilipwa Riyali 60 badala ya Riyali 100 ambazo wakala wake alimuahidi. Anasema mwajiri wake alimtaka kimapenzi lakini alipomkataa alimpiga.. Dar es Salaam, Tanzania.
©2017 Sophie Stolle
Rehema M., 30, alisema mwajiri wake huko Oman alimlazimisha kufanya kazi baada ya kuungua mkono alipokuwa anasafisha chupa ya chai iliyomlipukia. Dar es Salaam, Tanzania.
© 2017 Rothna Begum/Human Rights Watch
Mkalimani akionyesha kovu kichwani kwa “Basma N.” Basma alisema mtoto wa mwajiri wake aliwasha feni la juu wakati akiwa anasafisha juu ya kabati la vyombo. Feni ilimpiga kichwani kisha akaanguka chini. Huku akiwa anavuja damu nyingi kutokana na kuumia kichwani, alikimbilia ubalozi wa Tanzania. . Dar es Salaam, Tanzania.
© 2017 Rothna Begum/Human Rights Watch
Asma, 24, alisema kufuatia miezi kadhaa ya kutengwa na kunyanyaswa akiwa anafanya kazi kama mtumishi wa ndani huko Oman: “Nilijiskia kuchanganyikiwa.” Anasema ilimchukua miezi mingine mitatu kurudia hali yake ya kawaida baada ya kurudi Tanzania. Dar es Salaam, Tanzania.
© 2017 Rothna Begum/Human Rights Watch
“Amani W., 31, mtumishi wa ndani wa zamani alierudi kutoka Oman mwanzoni mwa 2017 baada ya kufanya kazi miaka mitatu na mwajiri ambae anasema alikuwa akimlazimisha kufanya kazi masaa mengi bila mapumziko au siku ya mapumziko. Sasa anashindwa kupata kazi, anafikiria kuuza samaki kujiingizia kipato au kuhama tena. Soko la samaki, Bagamoyo, Tanzania.
©2017 Rothna Begum/Human Rights Watch