Skip to cookie privacy notice
Skip to main content
Human Rights Watch
العربية
简中
繁中
English
Français
Deutsch
日本語
Русский
Português
Español
More
languages
Search
Donate Now
Search
العربية
简中
繁中
English
Français
Deutsch
日本語
Русский
Português
Español
More
languages
Would you like to read this page in another language?
Yes
No, don't ask again
✕
Close
February 14, 2017
Available In
English
Kiswahili
Nilikua Na Ndoto Ya Kumaliza Shule
Maafisa wa usalama waliokuwa wamejihami waliwatazama waandamanaji waliokuwa wakiandamana dhidi ya serikali wakati wa sherehe za kitamaduni za Irreechaa huko Bishoftu, Uhabeshi tarehe mbili Octoba 2016. © 2016 Getty Images
Mchoro nje ya ofisi za Shirika la Maendeleo ya Jamii la Rafiki, Wilaya ya Kahama, Shinyanga. Mchoro huu unalenga kuhamasisha kuhusu unyanyasaji wa kijinsia kwa watoto wa kike wakiwa njiani kwenda shule, unaonyesha mwanafunzi wa kike akikataa kupokea pesa kutoka kwa mtu mzima na kusema “Sidanganyiki”. © 2016 Elin Martínez/Human Rights Watch
Eileen (jina la bandia), 21, aliacha shule akiwa kidato cha pili baada ya shule yake kufanya upimaji wa mimba na maafisa wa shule na wazazi kugundua kwamba ni mjamzito. Kwa Tanzania, maafisa wa shule mara kwa mara huwapima wanafunzi wa kike mimba kwa lazima ikiwa ni hatua za kinidhamu kuwafukuza shule wanafunzi wenye mimba. © 2016 Elin Martínez/Human Rights Watch
Fimbo ya mianzi ambayo hutumika na walimu kuchapa wanafunzi darasani ikiwa juu ya dawati katika shule ya sekondari huko Mwanza, Kaskazini-Magharibi mwa Tanzania. Human Rights Watch waligundua kwamba walimu wengine huwachapa wanafunzi na fimbo au hata kwa kutumia mikono yao au vitu vingine. © 2016 Elin Martínez/Human Rights Watch
Msichana akionyesha alama miguuni kwake zilizotokana na kuchapwa viboko mara kwa mara na walimu shuleni kwake. Aliwaambia Human Rights Watch: “Tuna alama miguuni, wanatupiga mikononi, wanatupiga kichwani”. © 2016 Elin Martínez/Human Rights Watch
Frances (pseudonym), 21, struggled to pay for secondary school. She worked as a domestic worker to help pay her school fees: “From 8 a.m. to 2 p.m. I studied, then from 5 p.m. – 11 p.m. I worked [at her employee’s home] and I also worked over the weekends ... I got 30,000 shillings [US$14] per month … not enough to pay for school.” She failed the secondary school exam and dropped out of Form IV. © 2016 Elin Martínez/Human Rights Watch
Wanafunzi wa kike katika shule ya sekondari huko Mwanza, ambao ni walemavu wa macho, wakiongozwa na waalimu wao kushuka kilima kikali na chenye kuteleza. Wanafunzi hawa hutembea katika ardhi yenye milima na mabonde kutoka shuleni kuelekea katika mabweni ya shule. © 2016 Elin Martínez/Human Rights Watch
Mashine zilizokuwa zikitumika na wanafunzi wenye ulemavu wa macho zikiwa zimeharibika na kuweka katika kabati katika shule ya sekondari kwa watoto wenye ulemavu mkoani Shinyanga, kaskani mwa Tanzania. Shule nyingi za sekondari zinakosa vifaa vya msaada wa ufundishaji unaohitajika kuwezesha elimu kupatikana kwa wanafunzi wote kwa usawa. © 2016 Elin Martínez/Human Rights Watch
Maabara ya sayansi ambayo bado haijamalizika iliyopo karibu na darasa katika shule ya sekondari mkoani Shinyanga, kaskazini mwa Tanzania. © 2016 Elin Martínez/Human Rights Watch
Vyoo vilivyochakaa vya wanafunzi wa kike na kiume katika shule ya sekondari huko Mwanza, kaskazini-magharibi mwa Tanzania. Vyoo na miundombinu salama na ya kutosha ya usafi ni vitu vya msingi kwa mazingira ya elimu yanayokubalika, lakini katika shule nyingi za sekondari, vyoo havina hadhi. Wanafunzi wengi waliohojiwa na Human Rights Watch waliripoti kuwa wanatumia vyoo vichafu na kwa msongamano. © 2016 Elin Martínez/Human Rights Watch
Tangazo la “Kuongea Kiingereza” lilipo katika shule ya sekondari Ukerewe, kisiwa kilichopo Ziwa Victoria, Mwanza, kaskazini-magharibi mwa Tanzania. Shule nyingi za sekondari zinasisitiza matumizi ya kiingereza- lugha mpya kwa wanafunzi wa sekondari kwani Kiswahili ndiyo lugha ya kufundishia shule za msingi. Wanafunzi wengi hawapewi msaada wa kutosha kuendana na mabadiliko ya kutoka Kiswahili kwenda Kiingereza na wengine wanaripoti kuwa wanapewa adhabu kwa kushindwa kuongea Kiingereza darasani. Mwaka 2014, Serikali ilipitisha sera ya kukubali matumizi ya pamoja ya Kiswahili na kiingereza kama lugha za kufundishia kwa shule za sekondari. © 2016 Elin Martínez/Human Rights Watch
Zaidi ya wanafunzi 120 wa kidato cha pili wakijiandaa kufanya mitihani ya majaribio katika shule ya sekondari huko Mwanza, Kaskazini-Magharibi mwa Tanzania. © 2016 Elin Martínez/Human Rights Watch
© 2016 Elin Martínez/Human Rights Watch
Region / Country
Africa
Tanzania
Topic
Children's Rights
Education
Women's Rights
Gender Equality
Sexual Violence and Rape