Tangazo la “Kuongea Kiingereza” lilipo katika shule ya sekondari Ukerewe, kisiwa kilichopo Ziwa Victoria, Mwanza, kaskazini-magharibi mwa Tanzania. Shule nyingi za sekondari zinasisitiza matumizi ya kiingereza- lugha mpya kwa wanafunzi wa sekondari kwani Kiswahili ndiyo lugha ya kufundishia shule za msingi. Wanafunzi wengi hawapewi msaada wa kutosha kuendana na mabadiliko ya kutoka Kiswahili kwenda Kiingereza na wengine wanaripoti kuwa wanapewa adhabu kwa kushindwa kuongea Kiingereza darasani. Mwaka 2014, Serikali ilipitisha sera ya kukubali matumizi ya pamoja ya Kiswahili na kiingereza kama lugha za kufundishia kwa shule za sekondari.