Eileen (jina la bandia), 21, aliacha shule akiwa kidato cha pili baada ya shule yake kufanya upimaji wa mimba na maafisa wa shule na wazazi kugundua kwamba ni mjamzito. Kwa Tanzania, maafisa wa shule mara kwa mara huwapima wanafunzi wa kike mimba kwa lazima ikiwa ni hatua za kinidhamu kuwafukuza shule wanafunzi wenye mimba.