Zeinab Bulley Hussein akiwa ameshika kitambulisho cha Taifa cha mwanawe wa kiume, Abdi Bare Mohamed. Wanakijiji waliupata kwa ghafla mwili wa Abdi Bare yapata kilomita 18 kutoka Mandera, kaskazini mashariki mwa Kenya, wiki tatu baada ya maafisa wa polisi kumtia nguvuni nje ya nyumba ya familia yao mnamo Agosti 2015.