“Tuchukulie Kama Wanadamu”

Katika ripoti yenye kurasa 107 iliyopewa kichwa, “Tuchukulie Kama Wanadamu’: Ubaguzi dhidi ya Wafanyabiashara wa Ngono, Walio wachache Kijinsia (LGBTI), na Wanaotumia Dawa za Kulevya nchini Tanzania,” inaeleza ukiukaji kama mateso, ubakaji, kushambuliwa, kukamatwa kiholela, na kunyang’anywa pesa. Mashirika haya yaligundua kwamba hofu ya kukiukwa inawalazimu wafanyakazi wa ngono; watumiaji wa dawa za kulevya; na wanawake wanaofanya mapenzi na wanawake, wanaume wanaofanya mapenzi na wanaume, wanaovutiwa na jinsia zote mbili, wanaotamani kubadilisha jinsi zao, na watu wenye jinsia mbili (LGBTI) kwenda mafichoni mbali na huduma za kinga na matibabu. Makundi haya yalifanya utafiti wao kutoka mwezi wa Mei 2012 hadi Aprili 2013, na yaliwahoji wanachama 121 wa makundi yaliyo katika hatari kubwa, pamoja na maafisa wa serikali ya Tanzania, wahudumu, na wasomi.