Afrika Mashariki: Uhuru wa Kiraia Unapungua
Mlolongo wa ukandamizaji wa wazi wa serikali dhidi ya waandamanaji wa amani, wanaharakati, na waandishi wa habari uliibuka katika ukanda wote wa Afrika Mashariki na Pembe ya Afrika mnamo mwaka 2018, shirika la kutetea haki za binadamu Human Rights Watch limesema leo katika ripoti yake, Ripoti ya Ulimwengu ya 2019.