Tanzania: Watumishi wa ndani wahamiaji wanavyonyanyaswa huko Oman, UAE

(Dar es Salaam, Novemba 14, 2017)-  Watumishi wa ndani wa Kitanzania wanaofanya kazi Oman na Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) wanakumbana na saa nyingi za kazi, kutokulipwa mishahara, na unyanyasaji wa kimwili na kijinsia, haya yamesemwa na ripoti ya Human Rights Watch iliyotolewa leo. Sheria kandamizi za udhamini wa viza katika nchi hizo na mapungufu katika sera za Tanzania zinawaacha wanawake kupambana na unyonyaji.

News