Skip to main content

Kenya: Kutoweka kwa Watu, na Vifo katika eneo la Kaskazini Mashariki

Serikali Yafaa Kufanya Uchunguzi na Kuwahakikishia wote haki

(Nairobi) – Zaidi ya watu thelathini na wanne (34) wametoweka bila kujulikana walipo katika kipindi cha miaka miwili iliyopita. Watu hao walikamatwa na maafisa wa usalama wa Kenya wakati wa operesheni za kiusalama katika kupambana na ugaidi mjini Nairobi na Kaskazini Mashariki mwa nchi. Kwa mujibu wa shirika la kutetea haki za kibinadamu la Human Rights Watch, oparesheni hizo zilikumbwa na visa vingi vya ukiukaji wa haki za kibinadamu. Serikali ya Kenya yafaa ikomeshe ukiukaji wa haki za kibinadamu wakati wa operesheni za kukabiliana na vitendo vya ugaidi, na kuanzisha uchunguzi mahsusi mara moja, kuhusu vifo vya washukiwa na kutoweka kwa watu bila kujulikana waliko katika eneo hilo.

Zeinab Bulley Hussein akiwa ameshika kitambulisho cha Taifa cha mwanawe wa kiume, Abdi Bare Mohamed. Wanakijiji waliupata kwa ghafla mwili wa Abdi Bare yapata kilomita 18 kutoka Mandera, kaskazini mashariki mwa Kenya, wiki tatu baada ya maafisa wa polisi kumtia nguvuni nje ya nyumba ya familia yao mnamo Agosti 2015. © 2015 Will Swanson wa jarida la Washington Post inatumika kupitia Getty Images


Kwenye ripoti yake ya kurasa themanini na saba (87), yenye mada "Vifo na Kutoweka kwa Watu: Ukiukwaji wa Haki za Kibinadamu katika Operesheni za Kupambana na Ugaidi Mjini Nairobi na Kaskazini Mashariki mwa Kenya,” shirika la Human Rights Watch limenukuu matukio thelathini na nne (34) ambapo vikosi mbali mbali vya kiusalama vilihusika katika operesheni zilizoendeshwa na Jeshi la nchi lililotekeleza vitendo kama vile, kuvamia makaazi ya watu na kuwatia mbaroni watu ambao walidaiwa kuwa watuhumiwa, walio na uhusiano na kundi la wapiganaji wa kiislamu la Al-Shabab. Lakini miezi kadhaa baadaye, na hata mwaka mmoja baada ya operesheni hizo, watuhumiwa hao hawajashtakiwa mahakamani kwa kosa lolote, na jamii zao zimeshindwa kujua kule wapendwa wao waliko. Katika kila kisa, ingawa jamii za watuhumiwa ziliripoti kwa polisi kuhusu kutoweka kwa wapendwa wao na kutafuta usaidizi kutoka kwa vitengo mbali mbali vya serikali, mamlaka yalishindwa kuwafahamisha kule waliko washukiwa au kufanya uchunguzi wa kina kuhusu madai ya ukiukwaji wa haki za kibinadamu.

"Watu wa eneo la kaskazini mashariki mwa Kenya wanastahili kulindwa dhidi ya mashambulizi ya Al-Shabab, lakini sio unyanyasaji zaidi kutoka kwa maafisa wa serikali," alisema Ken Roth, Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Human Rights Watch. "Kuwatia nguvuni watu kiholela na kukataa kueleza kule wanakozuiliwa ni kosa kubwa la uhalifu, ambalo linachangia zaidi kuenea kwa uhasama na kutoaminiana baina ya vyombo vya usalama na watu."
 

Human Rights Watch lilifanya uchunguzi wa kina kwa muda wa zaidi ya miezi minane kubaini ukiukwaji wa haki za kibinadamu mjini Nairobi na katika kaunti za Kaskazini Mashariki mwa Kenya za Garissa, Wajir na Mandera. Shirika hili liliwahoji watu mia moja na kumi na saba (117 ) baadhi yao wakiwa ni waathiriwa, na watu walioshuhudia vitendo vya ukiukwaji wa haki za kibinadamu katika operesheni za kukabiliana na ugaidi, watu hao, wakiwa ni maimamu wa kiislamu, maafisa wa serikali, wanahabari, mawakili, wakereketwa wa haki za kibinadamu, maafisa wa Polisi na wakijeshi na viongozi wa mashinani katika eneo hilo. Shirika hilo pia lilifanya mahojiano ya udhibitisho zaidi mjini Nairobi, kupitia mazungumzo ya simu na waathiriwa na walioshuhudia visa hivyo katika eneo hilo la Kaskazini Mashariki.

Read a text description of this video

TEXT ON SCREEN
In April 2015, armed Islamist group Al Shabab attacked Garissa University College in northeastern Kenya killing 148 people. Al-Shabab has carried out dozens of other deadly attacks in Kenya in recent years. Kenyan authorities have cracked down and increased law enforcement operations, arresting many.

Adan, Brother of disappeared person:
Omar Yusuf was my older brother.  On April 26 of last year, he was picked up by two men from the anti-terror police unit.  This was the last time he was seen.
 

TEXT ON SCREEN
At least 34 people have been forcibly disappeared in Nairobi and northeastern Kenya in the last two years.


“Halima”, Relative of disappeared person
They did not tell me who they were but some of them were in plain clothes and some were dressed in police uniform. They put her in a Toyoto Probox, registration plate number KCC406Y and drove away with her. They said they were going to ask her questions and they would bring her back.
 

TEXT ON SCREEN
Counterterrorism operations have been marked by enforced disappearances, torture and arbitrary arrests.


Adan, Brother of disappeared person:
We don’t know whether he is alive or dead. There isn’t an office you can go to and enquire about him so it is very difficult.


“Halima”, Relative of disappeared person
They [the Pangani police] looked for her name in the incident book and said she was not on the list of people detained in that police station. They said they had not seen her. I also reported to Shauri Moyo police station. I told them of the date of her arrest and they said they hadn’t received any female detainees in their station on that date.
 

TEXT ON SCREEN
Kenyan authorities deny knowledge of the missing people’s whereabouts and refuse to acknowledge growing evidence of abuses by security forces.


Adan, Brother of disappeared person:
We are asking the government to produce him in court and charge him if he has committed a crime.
 

“Halima”, Relative of disappeared person
She has been disappeared in her own country. The government is silent about her whereabouts. No one knows whether she is dead or alive.
 

SCROLL OF NAMES OF THOSE MISSING

TEXT ON SCREEN
The Kenyan government should urgently provide information on the whereabouts of the disappeared people. Anyone in detention should be charged or released.

 


Usalama wa watu hawa thelathini na wanne (34) unatiliwa shaka zaidi, kutokana na visa kumi na moja (11) vya hapo awali katika kipindi cha miaka miwili iliyopita, ambapo maiti ya watu waliokamatwa na polisi kwa tuhuma za ugaidi imepatikana, na mara nyingi ikiwa katika maeneo yaliyo mbali na mahali walikokamatwa. Kwa mjibu wa Shirika la Human Rights Watch, polisi hawajachukuwa hatua yoyote kuchunguza vifo hivi. Katika kisa kimoja, mwili ulifukuliwa mjini Mandera baada ya shinikizo kutoka kwa uma, lakini Serikali haijafanya upasuaji wa mwili au uchunguzi wowote kubainisha chanzo cha kifo kama inavyotakikana kwa mujibu wa sheria za Kenya.

Shirika la Human Rights Watch liligundua kwamba baina ya wale wanaokamatwa kiholela katika operesheni ni pamoja na vijana wenye asili ya kisomali, maimamu na walimu wa dini ya kiislamu katika shule za dini maarufu kama Madrasa. Mwanzo walizuiliwa katika vituo vya kijeshi na kambi za muda za kijeshi zilizomo msituni katika eneo la Kaskazini Mashariki na maeneo mengine nchini Kenya.Kwenye matukio mengine, maafisa wa polisi waliwakamata watu na kisha kuwakabidhi kwa majeshi.

Mwanamme mwenye umri wa miaka arobaini na nane (48), aliiambia Human Rights Watch kwamba polisi walimtia mbaroni mwezi Mei mwaka wa 2015, na kumzuilia kwa siku mbili katika kituo cha polisi cha Wajir na kisha kumsafirisha hadi kwenye kambi ya kijeshi ya Wajir. Alisema kuwa badaye maafisa wa kijeshi walimkamata kakake mkubwa na kuwazuilia wote wawili kwenye kambi hiyo ya kijeshi. Maafisa wa kijeshi walimpiga mateke, kumzaba makofi na kumpiga na vifaa vyenye miale ya umeme ili akiri makosa, na badaye kumuachilia baada ya siku kumi na tano. Kakake bado hajulikani alipo hadi sasa.

Katika kisa kingine mnamo tarehe 21 mwezi wa Machi mwaka wa 2015, wanajeshi wanne walimkamata Abdiwelli Ibrahim Sheikh mwenye umri wa miaka ishirini na nane (28) akiwa nyumbani kwake na walioshuhudia walisema waliona akipelekwa kwenye kambi ya kijeshi mjini Mandera. Mwanamme huyu hajawahi kuonekana tena. "Maafisa wa usalama walisema walitaka kumhoji kwa kifupi tu kisha badaye wangemuachilia", alisema mwanamme mmoja mwenye umri wa miaka hamsini (50) ambaye alikuwa na Abdiwelli wakati alipokamatwa. "Hatukujua kwamba ingekuwa mara ya mwisho kumwona."

Jamaa wamewatafuta wapendwa wao kila mahali ikiwemo kwenye vituo vya Polisi. Wametafuta usaidizi wa viongozi wa kidini na wanasiasa katika juhudi za kuwapata, na hata mara nyingi kutumia mitandao ya kijamii kuwasaka watu wao. Baadhi ya jamaa walichukuwa hatua za kisheria za kuitaka mahakama iishurutishe Serikali kutoa habari kuhusu walipo wapendwa wao, (kupitia amri ya habeas corpus).Hata hivyo, maafisa wa usalama wamekanusha kufahamu mahali walipo watu waliokamatwa.

"Ikiwa Wakenya wanatoweka kiholela, ni jukumu la polisi kushirikiana na familia na walioshuhudia visa hivi ili kutafuta watu waliotoweka," Roth alisema. Aliongezea kwamba, " Hatua ya serikali ya kuwa kimya inatilia shaka."

Operesheni za kupambana na ugaidi zilianza katika eneo la Kaskazini Mashariki mwa Kenya baada ya shambulizi la kigaidi kwenye jumba la kibiashara la Westgate mjini Nairobi lililotokea mwezi Septemba mwaka 2013. Oparesheni hizo ziliendelezwa zaidi baada ya uvamizi wa kigaidi katika chuo kikuu cha Garissa mnamo mwezi Aprili mwaka wa 2015, ambapo watu mia moja arobaini na saba (147), wakiwemo wanafunzi mia moja arobaini na wawili waliuwawa. Wapiganaji wa kundi la Al-Shabab walikiri kutekeleza mashambulizi hayo mawili. Al-Shabab imekiri kutekeleza mashambulizi mengine ya kigaidi ya kinyama nchini Kenya hasa katika eneo la Kaskazini Mashariki.

Katika kukabiliana na mashambulizi haya, jeshi la Kenya, polisi, maafisa wa kitengo cha Ujasusi na askari wa kulinda wanyama pori (KWS), walipelekwa katika maeneo ya Kaskazini Mashariki, na pia kushirikiana na vitengo mbali mbali vya kiuslama mjini Nairobi.

Shirika la Human Rights Watch linaamini kwamba watu hao thelathini na wanne (34) ni waathiriwa wa kutoweka kwa lazima, hali ambayo inatambuliwa katika sheria za kimataifa kama hatua ya kunyimwa uhuru na vyombo vya serikali, ikiambatana na serikali kukataa kukiri kwamba iliwakamata au kuficha ukweli kuhusu hatma na mahali walipo watu hao. Juhudi za kupata usemi kutoka kwa idara ya polisi na jeshi kuhusu kutoweka kwa watu hawa thelathini na wanne (34) na wengine wasiojulikana walipo hazikufaulu.

Serikali ya Kenya imechelewa sana kuchukuwa hatua ya kuchunguza ukiukwaji wa haki za kibinadamu wakati wa oparesheni dhidi ya ugaidi, Shirika la Human Rights Watch limesema. Serikali inafaa itoe habari za kina kuhusu utambulisho, hatma na mahali walipo watu waliotiwa mbaroni wakati wa operesheni hiyo, na kuhakikisha sheria za nchi unafuatwa ili kutenda haki kwa kila mtu ambaye amekamatwa au yuko korokoroni.

Polisi na jeshi la Kenya yafaa waanzishe uchunguzi wa haraka kuhusu madai ya kutoweka kwa watu, unyanyasaji na vifo katika eneo la Kaskazini Mashariki mwa Kenya, na kuwachukulia hatua za kisheria wote wanaohusika na vitendo hivyo vya kinyama. Rais anafaa ateue tume maalum ya kuchunguza na kubaini ukweli wa mambo kuhusu ukiukwaji wa haki za binadamu wakati wa operesheni ya kupambana na ugaidi nchini Kenya.

"Ni wazi kwamba Kenya inakabiliwa na changamoto nyingi sana za kiusalama, lakini serikali ina wajibu wa kuitikia ipasavyo na kufuata ujumb wa kisheria kwenye operesheni yoyote halali,” Roth alisema. "Kutoweka kwa watu na vifo ambavyo havijachunguzwa katika eneo la Kaskazini Mashariki sio tu kinyume cha sheria bali visa hivyo vinaashiria hatari ya kutenga jamii ya eneo hilo, na kufanya hali iwe mbaya hata zaidi."

Baadhi ya vipengee kutoka kwa watu waliohojiwa katika ripoti:

"Walimueleza Omar kwamba walitaka kumuhoji  kuhusiana na usalama wa taifa na kisha wangemuachilia huru. Hawakujitambulisha lakini ni watu ambao wanajulikana kuwa maafisa kutoka Idara ya Upelelezi yaani CID, kwa hivyo Omar hakuwauliza wajitambulishe. Hiyo ilikuwa mara yetu ya mwisho kwetu kumuona"
– Mwanamme, jamaa wa Omar Yusuf ambaye alikamatwa mjini Mandera mwezi Aprili mwaka wa 2015.

"Maafisa wa Polisi waliwabeba watu watano na kuwarusha ndani ya magari aina ya Land Cruiser,yaliyokuwa na nambari za usajili zinazofanana na magari yanayotumiwa na majeshi yanayohudumu katika kikosi cha Umoja wa Afrika nchini Somalia (AMISOM) na kisha kuenda nao. Baadaye tulifahamishwa kutoka kwa watu waliowaaona magari hayo barabarani kwamba yalikuwa yakielekea upande wa Somalia.”
– Mwanamme mwenye umri wa miaka 50 ambaye alikuwepo wakati majeshi ya Kenya yalipovamia mkahawa mmoja mjini Garissa, huku wakifyatua risasi na kuwakamata wanaume watano akiwemo Hassan Abdullahi, ambaye hajulikinani mahali alipo.

"Maafisa wa polisi katika kituo cha Garissa hawajatupa usaidizi wowote na sidhani kama wanajali. Walituambia kwamba siku hiyo wao pia walisikia milio ya risasi lakini hawakufahamu nini kilichokuwa kikiendelea. Kamishna wa kaunti ya Garissa alituambia kwamba hakufahamu kile kilichotendeka lakini ilibainika wazi kwamba hakutaka kutusaidia. Afisa mmoja wa kitengo cha Jinai alituambia kwamba alijaribu kuwapigia polisi simu baada ya kusikia milio ya risasi ili aulize kile kilichokuwa kikiendelea. Baada ya dakika moja hivi, alipokea simu kutoka kwa nambari iliyofichwa ikimuamrisha aondoke mahala hapo mara moja na asidhubutu kuzungumzia kisa hicho tena.”
– Mwanamme mwenye umri wa miaka 25, ndugu ya mwanaume mmoja aliyetoweka.

"Kakangu alichukuliwa kutoka mji alikozaliwa, alikokua, ambako alikuwa na familia yake na kwa sasa hakuna anayejua kama angali hai au ameaga dunia. Kwa hivyo kila mtu anahisi uchungu wa kisa hiki. Kuona mwili wa jamaa yako ni uchungu lakini angalau umethibitisha kwamba amefariki.”
– Mwanamme ambaye nduguye hajaonekana tangu akamatwe na polisi mnamo Aprili 26, 2015.

Your tax deductible gift can help stop human rights violations and save lives around the world.

Region / Country