Kambi ya Nduta nchini Tanzania kwasasa inahifadhi wakimbizi na watafuta hifadhi wa Burundi wapatao 70,109. Takribani Warundi 154,000 wanaishi katika kambi tatu – Nduta, Nyarugusu na Mtendeli – kaskazini magharibi mwa Tanzania katika mkoa wa Kigoma, ambapo baadhi yao wamekumbwa na ukamataji holela, kupotezwa kwa nguvu, na kuteswa.