Wafanyakazi wasio raia huchangia asilimia 95 ya wafanyakazi wote wa nchini Qatar. Ndio wafanyakazi wanaojenga muundo msingi, hoteli, viwanja vya michezo, huku wakichangia pakubwa katika sekta ya huduma mbalimbali.