“Ruhiyyeh,” 17, kutoka jiji la Kolda, kusini mwa Senegali, alipata mimba akiwa mwaka wa mwisho wa shule ya sekondari ngazi ya chini. Mkuu wa shule na mwalimu wa shule ya sekondari walimhamasisha kurudi shule baada ya kujifungua, na sasa wanahakikisha anapata muda mtoto wake anapoumwa.