“Eileen, 23, aliacha shule akiwa kidato cha 2, mwaka wa pili wa shule ya sekondari ngazi ya chini, akiwa na miaka 17, wakati shule ilipofanya vipimo vya mimba na maafisa wa shule na wazazi wakagundua alikuwa mjamzito. Nchini Tanzania, maafisa wa shule mara kwa mara hufanya vipimo vya lazima vya mimba kwa wasichana kama hatua za kinidhamu kufukuza wanafunzi wajawazito shule.