“Angela,” 20, akitembea na mtoto wake karibu na nyumbani kwake baada ya kurudi kutoka shule katika kaunti ya Migori, magharibi mwa Kenya. Ni mwanafunzi wa Kidato cha 4 katika shule ya wasichana. Angela alipata ujauzito baada ya mwalimu wake aliekuwa katika mafunzo kujitolea kulipa sehemu ya ada yake ya shule ya msingi na kudai ngono kama malipo. Baba yake alitaka kumuozesha baada ya kujifungua, lakini Mama yake Angela alipingana na hili na kumsaidia kurudi shule. Anataka kwenda chuo na kusomea uuguzi.